Ibrahimovic amevunja rekodi ya Sven Rydel
aliyefunga mabao 49 Sweden
MSHAMBULIAJI wa PSG mabingwa wa soka
nchini Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic amefanikiwa kuvunja rekodi ya kuwa mchezaji aliyeifungia mabao
mengi zaidi timu ya taifa ya Sweden,baada ya kutupia mabao mawili usiku wa
kuamkia leo,ambapo Sweden imechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Estonia.
Mabao hayo mawili yanamfanya nyota
huyo mwenye umri wa miaka 32,kufikisha idadi ya mabao 50,akiipita idadi
iliyokuwa inashikiliwa na mchezaji Sven Rydell, ya kufunga mabao 49,na bao lake
la mwisho kati ya hayo akilifunga dhidi ya Finland mwaka 1932.
Baada ya kuvunja rekodi hiyo, alitoa
jezi yake kuonyesha ujumbe kwa mashabiki uliosomeka. "Ni gjorde det
mojligt,' or: wenye maana 'Umefanya iwezekane.'

No comments:
Post a Comment