Sturridge
Mshambuliaji Daniel
Sturridge,amesema amevunjika moyo baada ya kutupwa nje ya kikosi cha England
kitakachocheza mechi yake ya ufunguzi wa patashika ya kufuzu kutinga fainali za
Euro 2016 dhidi ya Switzerland keshokutwa jumatatu.
Sturridge, 25,atakuwa nje ya kikosi hicho
chini ya kocha Roy Hodgson,baada ya kuumia jana ijumaa wakiwa katika mazoezi na
klabu yake ya Liverpool kwenye dimba la St George'Park.
Chama cha soka cha Uingereza
FA,kimethibitisha kuwa mchezaji huyo wa Liverpool ataukosa mchezo huo wa kufuzu
utakaopigwa mjini Basel.
"kusema kweli nimevunjika sana moyo
kuona sitalitumikia taifa langu kwenye mchezo huo,lakini kwa mujibu wa
madaktari-nina matumaini ya kurejea uwanjani muda mfupi tu ujao kushirikiana na
wenzangu katika mechi zinazofuata,Ni maneno aliyoyaandika Sturridge kwenye
mtandao wa kijamii wa Tweeter.

No comments:
Post a Comment