Mshambuliaji mpya wa klabu ya fc Barcelona ya nchini Hispania
LUIS SUAREZ amesema amekuwa na wakati mgumu kuitazama timu yake hiyo ikicheza
pasipo kutoa msaada wake uwanjani.
SUAREZ hawezi kuitumikia timu hiyo kutokana na adhabu aliyopewa
na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kumng’ata meno beki wa timu ya
taifa ya italia GIORGIO CHIELLINI katika mashindano ya kombe la dunia 2014
nchini brazil.
Aidha mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 aliyetokea Liverpool
atakuwa nje ya uwanja mpaka October 25,na amesema itamlazimu kuwa mvumilivu kwa
kipindi hiki.

No comments:
Post a Comment