Golikipa namba moja wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya
ubelgiji THIBAUT COURTOIS amesema anataraji kusaini mkataba mpya atakaporejea
katika klabu yake baada ya mechi za kimataifa kumalizika.
COURTOIS ambaye aliitumikia klabu ya atletico madridi ya nchini
Hispania kwa misimu mitatu kwa mkopo amerejea katika klabu yake msimu huu na
kuonesha kiwango cha hali ya juu na kumuweka benchi golikipa mkongwe wa klabu
hiyo PETER CECH
Aidha kocha JOSE MOURINHO amesema anataraji kumpa mkataba wa
miaka mitano Courtois, mwenye umri mdogo baada ya kuonesha kiwango kizuri
katika mechi alizocheza.
No comments:
Post a Comment