Kocha wa timu ya taifa ya England ROY HODGSON
amewatetea wachezaji wa timu hiyo kutokana na mchezo mbovu waliuonesha katika
mechi ya kirafiki baina ya timu hiyo na timu ya taifa ya Norway uliopigwa
katika uwanja wa wembley na timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.
HODGSON alichukia baada ya kuulizwa kwanini timu
hiyo ilipiga mashuti mawili tu yaliyolenga goli na kujibu kuwa timu hiyo
umeundwa na wachezaji wengi wasio na uzoefu hivyo haiwezekani mchezaji
alieitumikia timu hiyo kwa mechi 4 mpaka 5 afanye makubwa kama aliyoyafanya
DAVID BECKHAM na mchezaji majeruhi kama PHIL JONAS kumfananisha na mkongwe kama
JOHN TERRY.
Aidha kocha huyo amesema anajua kuwa idadi ya
mashabiki wa taifa hilo inapungua kila siku lakini yeye anachojali
nikuhakikiksha timu hiyo inafanya vizuri na atahakikisha wanashinda mechi yao
dhidi ya Switzerland jumatatu ijayo.

No comments:
Post a Comment