RAIS WA REAL MADRID AKANUSHA KUWA NA UGOMVI NA RONALDO
Rais wa Madrid Florentino Perez akiwa na Ronaldo
Rais wa klabu ya Real
madridi FLORENTINO PEREZ amesema hakuna hali ya kutoelewana kati yake na
mshambuliaji wa klabu hiyo CRISTIANO RONALDO licha ya kuwepo kwa uvumi mbalimbali
kuhusu uhusiano wao kwa sasa.
Nyota huyo mapema wiki hii aliponda uamuzi uanaofanywa rais huyo wa
kuwauza wachezaji mahiri licha ya kuwa wametoa mchango mkubwa katika kikosi
hicho.
Aidha PEREZ ambaye
anapenda kusajili wachezaji wenye majina makubwa amesema kuuzwa kwa wachezaji
kama ANGEL DI MARIA ni uamuzi sahihi kutokana na hela iliyotolewa na klabu ya
Manchester united na XABI ALONSO ameuzwa kutokana na yeye mwenyewe kutaka
kuondoka.
No comments:
Post a Comment