mshambuliaji wa klabu ya West Ham,Andy Carroll,ameripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi minne baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu.
mchezaji huyo wa zamani wa vijogoo wa Liverpool,mwenye umri wa miaka 25,atafanyiwa upasuaji leo ijumaa huko United States.
Carroll amekumbwa na janga hilo katika ziara ya kikosi chake cha Hammers' huko New Zealand kwaajili ya maandalizi na kujipima nguvu kabla ya kuanza patashika ya ligi kuu ya England.
wakati akiwa mazoezini,alionekana kuchechemea na baadaye madaktari walipomfanyia uchunguzi wa awali,wakagundua kuwa mguu wake wa kushoto unahitaji kufanyiwa upasuaji kwa matibabu zaidi.

No comments:
Post a Comment