Navas akimzidi maarifa mshambuliaji wa timu pinzani na kumuachia manyoya
Golikipa Navas akiwapanga mabebi wake wakati akiwa na klabu ya Levante
Klabu ya Real Madrid,imekamilisha
usajili wa golikipa wa Costa Rica, Keylor Navas kwa mkataba wa muda mrefu
kuitumikia klabu hiyo ya Hispania.
Navas aliyeifikisha Costa Rica hadi
hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza katika historia yake huko nchini Brazil,amekubali
kuingia mkataba wa miaka 6.
Mlinda mlango huyo,27-ametua Santiago
Bernabeu akitokea kunako klabu ya Levante ambayo nayo inashiriki ligi kuu ya
Hispania maarufu kama La Liga.
Baada ya kukamilisha usajili
huo,Madrid itamtambulisha Navas mbele ya mashabiki wake kesho jumanne mara tu
baada ya kukamilisha zoezi la vipimo vya afya yake.
Navas sasa atakuwa anagombania namba
pamoja na magolikipa wenzake aliowakuta, Iker Casillas na Diego Lopez.
Huyo anakuwa mchezaji wa tatu
kujiunga na Real Madrid ambao ni mabingwa wa ulaya,baada ya kuwasajili mjerumani-Toni
Kroos na MColumbia- James
Rodriguez.



No comments:
Post a Comment