Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers,amepuuza taarifa za yeye kumuhitaji mshambuliaji mtukutu wa AC Milan, Mario Balotelli,baada ya kuwepo tetesi za kumuwinda nyota huyo wa timu ya taifa ya Italia.
Daily Mirror
Tottenham ipo tayari kutoa kitita cha pauni milioni £17m kwaajili ya kumsajili beki wa kati wa klabu ya Villarreal na timu ya taifa ya Argentina,Mateo Musacchio,23.
Times (subscription required)
Kocha wa West Ham United, Sam Allardyce,anammezea mate mshambuliaji wa Manchester United, Wilfried Zaha, 21,kumshusha Upton Park.
Mbali na mchezaji huyo,pia Spurs wanahitaji huduma ya mshambuliaji ngongoti wa Stoke City- Peter Crouch, 33, ili kuziba pengo la Andy Carroll aliye majeruhi.
Lakini hata hivyo mshambuliaji wa Sunderland Connor Wickham, 21,amewekwa katika chaguo la kocha Allardyce,kuziba pengo la Carroll ambaye atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi 4.
Daily Telegraph
Meneja wa Southampton,Ronald Koeman yu tayari kumsajili kind la Manchester United mshambuliaji Demetri Mitchell,17 kwa mkopo.
Daily Mirror
Klabu ya Italia AC Milan,imeonesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Liverpool Pepe Reina,31-lakini kiwango kikubwa cha mshahara anaoutaka kipa huyo huenda kikakwamisha kabisa mpango huo.
Daily Mail

No comments:
Post a Comment