WATANZANIA bado wanaendelea kuuguza donda lisilopona katika medani ya soka,huku wakijiuliza maswali magumu yasiyojibika kila kukicha kwamba ninani anayeliroga taifa hili lisifanye vizuri katika michuano ya kimataifa?
Swali hilo hakuna mtanzania yeyote anayeweza kujibu isipokuwa
wapo wachache mwenye kujaribu kutoa maelezo yenye kutafuta mwarobaini wa tatizo
hilo.
Starz ilipata bahati ya kuingia katika kinyang’anyiro cha
kuwania tiketi ya kucheza michuano ya kuwania kombe la mataifa ya afrika
itakayofanyika mwakani kule nchini Moroco,lakini cha kushangaza imeshindwa
kuonesha kama inaweza kushiriki katika michuano hiyo.
Mechi yake ya kwanza dhidi ya Zimbabwe starz ilijitahidi
kufurukuta na kufanikiwa kuisukumiza nje Zimbabwe katika patashika hizo na
kusonga mbele kuvaana dhidi ya Mambaz wa Msumbiji ikiwa ni hatua ya mwisho
kabla ya kuvuka na kuingi akatika hatua ya makundi,lakini ikajikuta inapepesa
macho katika mchezo wa kwanza uliopigwa hapa nyumbani kwa kulazimishwa sare ya
mabao 2-2.
Hata hivyo matokeo hayo hayakuivunja mioyo ya watanzania wengi
ambao walijipa matumaini kwamba wanaweza kupata ushindi wakiwa ugenini katika
mchezo wa marudiano lakini imekuwa tofauti.
Katika uwanja wa Zimpeto huko Msumbiji,Starz imejikuta ikikubali
kipigo cha mabao 2-1 na hivyo kuzima kabisa ndoto za taifa hili kucheza
michuano hiyo mikubwa barani afrika.
Hapana shaka kwa hali hii jinsi ilivyo,rais wa shirikisho la
kandanda la Tanzania TFF Jamal Emil Malinzi,anawajibika kubeba lawama za taifa
hili kufanya vibaya katika patashika hizo kutokana na maandalizi yasiyokuwa ya
kitaalamu kabla starz haijashuka dimbani.

No comments:
Post a Comment