WABEBA mitutu wa jiji la London Arsenal wanajiandaa kuishawishi klabu ya Paris
Saint Germain kwa kuwapa kitita cha pauni milioni 32 pamoja na kumtoa mchezaji Olivier
Giroud ili wampate mshambuliaji wao Edinson Cavani.
Cavani amewekwa katika nafasi za juu za wachezaji wanaotakiwa na kocha wa
the Gunners, Arsene Wenger,na hii ni baada ya nyota huyo wa Uruguway kuamua
kuiacha PSG msimu huu.
Bado haijafahamika kama PSG watakubali ofa hiyo ya Arsenal hasa ikizingatiwa
kuwa mshambuliaji wao nyota Zlatan Ibrahimovic amekuwa majeruhi tangu mwishoni
mwa wiki.
No comments:
Post a Comment