Friday, August 22, 2014

ARSENAL IMEMTENGEA PAUNI ML.10 ALEX SONG ATUE EMIRATES.

Wenger akiteta jambo na Song

Alex Song ameripotiwa yu mbioni kurejea kwenye klabu yake ya zamani Arsenal,baada ya kocha Arsene Wenger kuonesha nia ya dhati kutaka kumsajili tena kiungo huyo.

Song tayari ameshamwambia Wenger kwamba anaweza kuachana na Barcelona msimu huu kwa dau la pauni milioni 10,kutokana na kutokuwa katika mipango ya kocha  mpya Luis Enrique.

Liverpool ilikuwa nusura impate Song wiki iliyopita lakini gazeti moja la El Mundo Diportivo linaandika kwa sasa Arsenal ndio wanaoongoza mbio za kuinasa saini yake,baada ya kocha Wenger kumuwashia taa ya kijani ili atue Emirates.

Arsenal inahitaji kiungo mkabaji pamoja na beki wa kati nafasi ambazo Alex Song anaweza kuzitumikia,na wakala wa mchezaji huyo anafikiria juu ya mshahara atakaolipwa mchezaji wake.

Mpaka sasa hakuna mazungumzo yeyote kati ya Barcelona na Arsenal yaliyofikiwa kuhusu kuhama kwa Song,lakini mchezaji huyo anaweza kuondoka Barcelona wiki chache zijazo.
 


No comments:

Post a Comment