KIKOSI cha Real Madrid kimeshikishwa
adabu na wapinzani wao Atletico Madrid kwa kuchapwa bao 1-0 katika mchezo wa
fainali ya michuano ya kuwania Super Cup,mchezo uliopigwa usiku wa ijumaa.
Itakumbukwa kuwa katika mchezo wa
kwanza uliopigwa kunako dimba la Camp Nou,timu hizo zilikwenda sare ya
kufungana bao 1-1,na matokeo hayo yanaifanya Atletico kuchomoza na ushindi wa
jumla wa mabao 2-1.
Mfungaji aliyepeleka kilio kwa Madrid
ni Mario Mandzukic,aliyejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich,bao ambalo
amelifunga katika dakika ya pili tu ya mchezo.

No comments:
Post a Comment