Everton inategema kupata huduma
nzuri toka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto'o ,aliyejiunga na klabu hiyo kwa
mkataba wa miaka miwili.
Nyota huyo aliyetemwa msimu uliopita
na kocha Jose Morinho kwa madai kuwa umri wake umekwenda,ilikuwa asajiliwe na
Liverpool lakini dili hilo halikufanikiwa kutokana na klabu hiyo ya Vijogoo
kuvutiwa zaidi na mshambuliaji mtukutu Super Mario Balotelli.
Etoo huenda akashuka dimbani kuitumikia
klabu yake hiyo mpya katika mchezo wa ligi dhidi ya Chelsea utakaopigwa siku ya Jumamosi.
Mshambulizi huyo ambaye aliwahi kuwa
mchezaji nyota barani Afrika kwa miaka minne aliifungia Anzhi Makhachkala mabao
12 katika mechi 35 alizoshiriki.
Amewahi kuvitumikia pia vilabu vya
ligi kuu ya Hispania Real Madrid na Barcelona,na wakati akiwa huko Nou Camp, alitwaa ubingwa wa ligi ya Ulaya
mara mbili katika mwaka wa 2006 na 2009 .
Itakumbukwa kwamba Eto'o alijiunga
na Inter Milan 2009 kutokea Barcelona alipoisaidia kutwaa kombe la mabingwa
chini ya Mourinho huko San Siro.
Everton tayari wamemsajili Romelu
Lukaku kutoka Chelsea kwa gharama ya pauni milioni £28,pamoja na Christian Atsu wa mkopo.



No comments:
Post a Comment