Manchester United imekubali kulipa ada ya kuvunja rekodi ya
usajili wa klabu hiyo ya pauni milioni 59.7,kumsajili winga wa Real Madrid,
Angel Di Maria.
MuAgentina huyo mwenye umri wa miaka , 26,tayari amewasili mjini Manchester
kwaajili ya kukamilisha zoezi la vipimo vya afya yake leo jumanne asubuhi,na
kama akifaulu zoezi hilo atajiunga na klabu hiyo ya Old Traford ambayo itakuwa
imetumia kitita cha jumla ya pauni milioni 132 kwa usajili msimu huu.
Kiasi cha pesa kitakacholipwa na united kumsajili Maria-kinazidi ada
aliyosajiliwa nayo mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres,ambapo Chelsea
iliilipa Liverpool kiasi cha pauni milioni 50 mwaka 2011.
Usajili wa mwisho wa klabu hiyo wa gharama kubwa ilikuwa wakati ikimsajili
mchezaji Rio Ferdinand ambapo united imeilipa klabu ya Leeds kiasi cha pauni
milioni 29 mwaka 2002.
Mpaka sasa Manchester United imeshawasajili beki wa kushoto Luke Shaw,kiungo
Ander Herrer pamoja na mchezaji mwenza wa Angel Di Maria toka Argentina-Marco
Rojo,ambao wote wameigharimu United kitita cha pauni milioni 72 msimu huu.
Taarifa zinaripoti kuwa huenda akashuka dimbani jumamosi hii wakati United
ikishuka dimbani kukipiga dhidi ya Burnley katika patashika ya ligi kuu ya
England.
No comments:
Post a Comment