Uongozi wa klabu ya Dar Young Africans bado unaendelea
kupepesa macho na kung'ata maneno kuhusu hatima ya mshambuliaji wao mganda Emanuel
Okwi,ambaye amekuwa akiwasumbua tangu alipojiunga na klabu hiyo ya jangwani.
Taarifa toka kwa katibu mkuu wa yanga Beno Njovu,imesema
nyota huyo aliyerejea hivi karibuni toka nyumbani kwao Uganda hatokwenda
kujiunga na wenzake walioweka kambi huko Zanzibar na badala yake ataendelea
kubaki jijini mpaka wenzake watakaporejea.
Mpaka sasa uongozi wa yanga haujatoa uamuzi ni
mshambuliaji gani watakayemfungashia virago kati ya Emanuel Okwi na Hamis Kiiza
wote toka nchini Uganda,wakidai kuwa jukumu la kusema ninani abaki kwenye
kikosi hicho lipo mikononi kwa kocha wao mpya M-brazil Maxio Maximo.
Okwi alisajiliwa na yanga kwa ushawishi wa Hamis Kiiza
ambaye alifikisha asilimia 98 za kutimuliwa kwake huku klabu hiyo ikiwa haijui
ni vipi watampata Okwi,na baadaye Kiiza kudai kuwa yeye anauwezo wa kumshawishi
mganda mwenzie kuja kujiunga na yanga, lakini kwa mashariti kwamba mpaka naye
apewe mkataba ndipo afanye kazi hiyo.
Baada ya Okwi kuwasili na kiiza kupewa mkataba,uongozi wa
jangwani chini ya mwenyekiti wake Yusuph Manji,kwa sasa unaonesha wazi kuwa
hautaki kubaki na wachezaji wote kwa pamoja na badala yake wanataka
kutema mmoja wao,na kwa mujibu wa taarifa ilizoifikia blog hii ni kwamba kiiza
yupo karibu zaidi na mlango wa kutokea.
Yanga ipo kambini huko Zanzibar kwaajili ya maandalizi ya michuano ya ligi kuu,na watashuka dimbani kukipiga dhidi ya Mabingwa Azam FC kuwania ngao ya jamii.
Yanga ipo kambini huko Zanzibar kwaajili ya maandalizi ya michuano ya ligi kuu,na watashuka dimbani kukipiga dhidi ya Mabingwa Azam FC kuwania ngao ya jamii.
No comments:
Post a Comment