Shirikisho la soka la IVORY COAST,lipo njia panda kuamua kama
watacheza mechi yao ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya afrika dhidi ya
wapinzani wao SIERRA LEONE au la,kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Mechi hiyo muhimu kwa pande zote mbili,imepangwa kuchezwa
jumamosi ya septemba 6 mwaka huu,huko mjini Abidjan,lakini taarifa toka
serikali ya Ivory Coast inasema maafisa wa afya wan chi hiyo,wanaweza wakati
wowote kutangaza kuipiga marufuku mechi hiyo,kutokana na ukweli kwamba mataifa
5 ya kanda ya Afrika Magharibi yamekumbwa na ugonjwa huo wa Ebola ikiwemo Sierra
leone yenyewe.
SIERRA LEONE imeagiza maafisa wote wa ukufunzi kufanyiwa
uchunguzi wa kutosha kabla ya kuingia IVORY COAST na Tayari SIERRA LEONE
imetaja kikosi cha wachezaji wanaocheza nje ya Sierra Leone ilikuepusha hatari
ya kueneza Ebola IVORY COAST.
Kwa upande wake Shirikisho la soka barani Afrika CAF limekataa kufanya
mabadiliko yeyote ya mechi hiyo,na kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo
huenda Ivory Coast ikachukuliwa hatua ingawa haijulikani kama CAF watafanya
hivyo.

No comments:
Post a Comment