Messi akipokea tuzo ya mchezaji bora wa dunia-204 kwa mshangao
Siku
chache baada ya Mshambuliaji nyota wa klabu ya REAL MADRID na timu ya taifa ya
Ureno CRISTIANO RONALDO,kupokea tuzo ya kuwa mchezaji bora barani ulaya,nyota
huyo amemkejeli nyota nyota mwenzake wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina
LIONEL MESSI, kwa kusema kuwa mshambuliaji huyo hakustahili kupewa tuzo ya
mchezaji bora wa mashindano ya kombe la dunia ya mwaka huu yaliyomalizika huko nchini
Brazil.
RONALDO
alinukuliwa akisema,’nikisema kila kitu naweza kuchukuliwa hatua na kupelekwa
gerezani,lakini ukweli ni kwamba Messi hakustahili kupewa tuzo’alisema Ronaldo.
Wadadisi
wa mambo wamesema kauli hiyo inaweza kuamsha uhasama wa maneno kati ya
wachezaji hao wawili walio bora duniani,licha ya wao wenyewe kusema kuwa hawana
ugomvi wowote.
Messi
hakuonesha uwezo mkubwa katika mashindano hayo ya dunia,sambamba na Ronaldo
mwenyewe,lakini akajikuta akikabidhiwa tuzo hiyo iliyomfanya hata yeye mwenyewe
kuishangaa.
Mchawi
huyo mweupe wa soka duniani, alipewa tuzo hiyo baada ya kuwapiku wapinzani wake
THOMAS MULLER na mfungaji bora wa mashindano hayo JAMES RODRIGUEZ,baada ya
kufanikiwa kuweka nyavuni mabao 4.


No comments:
Post a Comment