Kocha
wa Liverpool Brenden Rodgers, amemuonya mshambuliaji wake mpya kutoka AC Milan mtukutu
Super Mario Balotelli,kwamba klabu haitokuwa tayari kumfiria yeye tu hivyo
anatakiwa kufuata taratibu na sheria toka kwa viongozi wake.
Kocha
Rodgers, amesema anajua kuwa Balotelli ni mchezaji mkubwa na mwenye kipaji na
anatakiwa kudhihirisha ubora wake kwa kuonesha kandanda zuri pamoja na
ushirikiano kwa viongozi pamoja na wachezaji wenzake aliowakuta.
Liverpool
imemsajli Balotelli hivi karibuni ili kuziba pengo lililoachwa na mshambuliaji
Luis Suarez,aliyejiunga na klabu ya Barcelona ya Hispania.
Tayari
nyota huyo ameshaanza kuwa gumzo katika maeneo mbalimbali huko Uingereza kutokana
na vituko vyake ndani na nje ya uwanja.

No comments:
Post a Comment