Baada ya kukosa nafasi ya kuwa kocha
msaidizi katika klabu ya Manchester united, mchezaji wa zamani wa klabu ya FC
Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi, Patrick Kluvert,sasa
ameelekeza nguvu zake kuomba nafasi ya kuwa kocha mkuu wa klabu ya Ross County
ya nchini Scotland.
Mwenyekiti wa klabu hiyo
Roy MacGregor amethibitisha kuwa Kluvert ni miongoni mwa makocha walioleta
maombi ya kutaka kuinoa klabu hiyo,lakini atakutana na upinzani mkali kutoka
kwa kocha wa zamani wa klabu ya St Mirren ambaye naye anahitaji nafasi hiyo.
Kluvert ,alikuwa kocha
msaidizi katika timu ya taifa ya uholanzi katika mashindano ya kombe la dunia
nchini brazil chini ya kocha Luis Van Gaal anayeinoa Manchester united.

No comments:
Post a Comment