Kocha aliyeipa ubingwa wa kombe la dunia timu
ya taifa ya Argentina mwaka 1978, Luis Menotti, amesema kocha wa zamani wa
klabu ya Barcelona ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Bayern Munich Pep Guardiola
,atakuwa kocha wa Argentina kama taifa hilo litaonesha nia ya kumuhitaji.
Menotti, amesema
alizungumza na kocha huyo raia wa Hispania na akamwambia kuwa anatamani kuwa
kocha wa taifa hilo ingawa anahisi viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu
nchini Argentina hawatapenda aina ya ufundishaji wa Guardiola.
Argentina haijapata
kushangilia ubingwa wa kombe la kopa Amerika tangu mwaka 1993 na Menotti
anaamini kuwa timu hiyo itanyakua ubingwa huo mwakani ikiwa chini ya kocha Guardiola.

No comments:
Post a Comment