Wednesday, September 3, 2014

IVORY COAST YAJITOA MUHANGA KWA EBOLA ,YAKUBALI KUCHEZA JUMAMOSI DHIDI YA SIERA LEONE

                                                                      Kikosi cha Tembo wa Ivory Coast

Shirikisho la soka la IVORY COAST,kwa idhini ya serikali ya nchi hiyo,imekubali kucheza mechi yake ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya afrika dhidi ya wapinzani wao SIERRA LEONE.

Awali Ivory Coast ilitishia kukataa kucheza mechi hiyo kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola,baada ya kuzingatia kwamba nchi za afrika magharibi zilizoripotiwa kukumbwa na ugonjwa huo mbaya,Siera Leone nayo imo.

Hata hivyo licha ya kuwemo kwa tishio hilo la Ebola,shirikishoa la soka barani afrika CAF,lilishikilia msimamo wake kwamba mechi hiyo ni lazima ipigwe huko Abidjan nchini Ivory Coast kama ilivyopangwa.

Mechi hiyo muhimu kwa pande zote mbili,imepangwa kuchezwa jumamosi ya septemba 6 mwaka huu,lakini hapo kabla SIERRA LEONE iliagiza maafisa wote wa ukufunzi kufanyiwa uchunguzi wa kutosha kabla ya kuingia IVORY COAST.

No comments:

Post a Comment