Wakati ligi kuu soka tanzania bara ikitaraji kuanza kutimua nasi za viwanja mbalimbali Septemba 20, mwaka huu,shirikishao la kandanda nchini TFF,limesogeza mbele kwa siku moja tarehe ya kuchezwa mchezo wa ngao ya jamii kuashiria kuanza kwa ligi hiyo.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa tff,Yoas Mwesigwa Selestine,ni kwamba mchezo Sasa uliokuwa upigwe septemba 13,sasa utapigwa siku inayofuata yaani jumapili ya septemba 14,katika dimba la taifa kuanzia saa kumi jioni,ukiwakutanisha mabingwa wa ligi Azam FC dhidi ya ya makamu bingwa Dar Youg Africans..
Baada ya kufunguliwa kwa ligi hiyo,septemba 20 kivumbi kitaanza kwa mabingwa watetezi, Azam FC ambao watakipiga dhidi ya Polisi Morogoro Uwanja wa Azam Complex, Chamazi,huku mwenyewe Yanga SC wakikipiga dhidi ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Mbeya City vs JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Sokoine, Mbeya,Simba SC vs Coastal Union
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Septemba 21.
Stand United vsNdanda ya Mtwara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mgambo JKT vs Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting vs Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

No comments:
Post a Comment