KIUNGO wa Real Madrid,Sami Khedira,atakuwa
nje ya kikosi cha taifa lake la Ujerumani kitakachocheza dhidi ya Argentina na
baadaye Scotland,kutokana na kupata majeraha.
Shirikisho la kandanda nchini
Ujerumani,limethibitisha jana kwamba mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja
kutokana na matatizo hayo.
Kocha mkuu wa Ujerumani,Joachim
Loew,tayari amemuita kiungo wa klabu ya Hoffenheim Sebastian Rudy ,ambaye atashuka dimbani na
kikosi hicho usiku wa leo kuziba pengo hilo la kiungo mkabaji.
Rudy, 24, alikuwemo
katika kikosi cha Ujerumani kilichotoka sare ya bila kufunga dhidi ya Poland katika mchezo wa kirafiki uliopigwa mei
13 kabla ya kuanza patashika ya michuano ya kombe la dunia.
Naye mlinzi ,Jerome
Boateng wa Bayern Munich pamoja
na Mats Hummels wa
Dortmund,pia hawatakuwemo kwenye kikosi cha kocha Low,kutokana na
kupata majeraha jana wakiwa katika mazoezi,lakini kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil,naye akienguliwa mapema kwenye
kikosi hicho kutokana na kuumia kifundo cha mguu.
Lakini hata hivyo,nahodha mpya wa
Ujerumani,Bastian Schweinsteiger naye
ameripotiwa kusumbuliwa na goti, huku Philipp Lahm, Miroslav
Klose na Per Mertesacker,wakiwa
tayari wamestaafu kuitumikia timu hiyo ya taifa,nah ii inamaanisha kuwa
Ujerumani huenda ikakwaa kisiki mbele ya Argentina,ambayo
ilifungwa katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia huko brazil.

No comments:
Post a Comment