WAKONGWE Miroslav
Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker wamepewa tuzo za heshima usiku huu kabla
ya mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Argentina Uwanja wa Esprit Arena.
Watatu hao waliichezea
Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla
ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
Klose, ambaye ni
mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani kwa mabao yake 71, ametungika daluga
baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
MCHANGO WAO KATIKA TIMU YA TAIFA UJERUMANI...
Miroslav Klose (Lazio)
- Mechi 137, mabao 71
Philipp Lahm (Bayern
Munich) - Mechi 113, mabao 5
Per Mertesacker
(Arsenal) - Mechi 104, mabao 4

No comments:
Post a Comment