RAFAEL NADAL
Matumaini ya Bingwa namba mbili wa mchezo wa Tenis duniani,Rafael
Nadal,kupona haraka jeraha la kifundo cha mkono wake yameyeyuka baada ya
adaktari wake kusema kwamba itamchukua muda wa siku kadhaa kupona jeraha hilo.
Nadal alilazimika kujiondoa katika mashindano ya US Open
kutokana na jeraha hilo la kifundo cha
mkono wa kulia,na hivyo kuwafanya mashabiki wake kukosa uhondo walioutegemea
toka kwa manatenesi wao mashuhuri.
Nyota huyo alipata jeraha alipokua kwenye mazoezi mwezi julai hali
iliyomfanya kushindwa kuhudhuria mechi mbili za kujipima nguvu.
No comments:
Post a Comment