Sunday, August 17, 2014

SUAREZ KUSHUKA DIMBANI LEO USIKU KUIKABILI CLUB LEON

Suarez akiwa mazoezini na wenzake
                                    Suarez tayari kwa kushuka dimbani leo usiku


Kocha wa Barcelona,Luis Enrique,amesema kuwa mshambuliaji wake mpya aliyemnunua toka Liverpool- Luis Suarez ,atashuka dimbani leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa kandanda nchini Mexico-Club Leon.


Suarez aliyekuwa akijifua vilivyo ili kubaki katika kiwango chake kilichowavutia Barcelona kiasi cha kumnunua kwa kiasi kikubwa cha pesa,atashuka dimbani hii leo lakini kwa mujibu wa kocha wake,hatoweza kumaliza dakika zote 90.

Nyota huyo raia wa Uruguway,hivi karibuni amekumbana na adhabu ya kutojihusisha na kandanda baada ya kumng'ata meno mchezaji wa timu ya taifa ya Italia,katika patashika ya kombe la dunia huko Brazil.


Itakumbukwa pia mwaka uliopita Suarez alilazimika kuomba radhi kutokana na kitendo chake cha kumng’ata meno beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic na kukumbana na adhabu ya kutocheza mechi 10.

Desemba mwaka 2011,alifungiwa kutocheza mechi 8 na kupigwa faini ya pauni elfu 40 kwa kuonesha ubaguzi dhidi ya mchezaji wa Manchester United, Patrice Evra, na mwezi novemba mwaka 2010,alifungiwa kutocheza mechi 7 kwa kumng’ata bega mchezaji wa PSV Endhoven-Otman Bakkal wakati akiichezea klabu ya Ajax.



No comments:

Post a Comment