Mshambuliaji Daniel Sturridge,amefunguka
na kusema kuwa klabu yake ya Liverpool ipo imara msimu huu hata bila ya kuwepo
mshambuliaji nyota mtukutu Luis Suarez,muda mchache tu baada ya kuisambaratisha
mabao 2-1 klabu ya Southampton katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo Liverpool
walitawala kipindi chote cha kwanza na kufanikiwa kupata bao katika dakika 23
likifungwa na Raheem Sterling kabla ya
mchezaji Clyne kuisawazishia klabu yake katika dakika 56,na baadaye Daniel
Sturridge katika dakika ya 79 akapigilia msumari wa mwisho kwa kuandika bao la
pili na la ushindi.
Sturridge ametoa kauli hiyo
alipoulizwa kama Liverpool itakuwa bora msimu huu licha ya kumuuza Suarez,na
kusisitiza kuwa kutokana na wachezaji waliowanunua msimu huu,hakuna ubishi
kwamba kikosi hicho sasa ni moto wa kuotea mbali.
Liverpool mpaka sasa msimu
huu,imewasajili beki Javier
Manquillo, 20,kwa mkopo akitokea kunako klabu ya Atletico Madrid,mshambuliaji
Divock Origi, 19, aliyetokea klabu ya Lille ya Ufaransa pamoja na
mlinzi Alberto Moreno, 22,aliyesajiliwa kutoka klabu ya Sevilla.
|
Wengine ni, Rickie Lambert,
32,na Adam Lalana,25 waaliyesajiliwa kutoka klabu ya Southampton, kiungo Emre
Can, 20, toka Bayer Leverkusen ya Ujerumani,Wingea Lazar Markovic,
20, toka klabu ya Benfica ya Ureno pamoja na mlinzi Dejan Lovren, 25,toka
klabu ya Southampton.
Usajili wa wachezaji wote hao umeigharimu Liverpool kitita cha pauni milioni 101.


No comments:
Post a Comment