Aguero
Silva
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya
England Manchester City,wameanza vema utetezi wao baada ya kuionesha kandanda
la uhakika klabu ya Newcastle United waliokuwa nyumbani kwao,kwa kuitandika
mabao 2-0 na kujikusanyia pointi zote tatu muhimu.
Bao la kwanza limepatikana katika
kipindi cha kwanza likifungwa na mchezaji David Silva katika dakika ya 39 baada
ya kupokea pasi murua toka kwa Eden Dzeko,kabla ya mshambuliaji Sergio Aguero
katika dakika ya 90 hajakwamisha mpira wavuni na kuandika bao la pili.
Ushindi huo unaonesha matumaini kwa
City kufanya vizuri katika msimu huu na kulitetea tena taji lake,licha ya
kushindwa kunyakua taji la ngao ya hisani mbele ya Arsenal katika mchezo wa
ufunguzi wa ligi.
Kocha Manuelle Pellegrini,amesema
hana wasiwasi hata kidogo na kikosi chake alichokisuka vema,na ana uhakika kuwa
safu zake zote zipo tayari kwa mapambano ya ligi.


No comments:
Post a Comment