ALIYEKUWA kocha wa Manchester United
David Moyes,anaamini kwamba hakupewa muda wa mutosha kuiongoza klabu hiyo kabla
ya kufukuzwa.
Moyes alichukua mikoba ya kuifundisha United
toka mikononi mwa kocha wa heshima Sir Alex Ferguson mwezi julai mwaka jana na
kufungashiwa virago mwezi April baada ya kuiweka Timu katika nafasi ya saba
kwenye msimamo wa ligi.
Nimekuwa nikiongeza mara nyingi na
Alex Ferguson tangu nilipofukuzwa nikizungumza naye kuhusu muda mchache niliopewa
kukaa na kikosi,na akafafanua kuhusu hilo na amekubali kuwa ni kweli nafasi
hiyo ilikuwa ngumu mno ikisababishwa pia na kukosa kuungwa mkono na mashabiki
waliokuwa akiyatolea macho matokeo pekee.
|

No comments:
Post a Comment