Sunday, August 17, 2014

KIUNGO WA EVERTON-BARKLEY OUT MIEZI MITANO


             Ross Barkley

KIUNGO wa Everton,Ross Barkley,ameripotiwa kwamba atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na kuumia kifundo cha mguu.


Kocha wa Everton-Roberto Martinez,amesema Barkley,mwenye umri wa miaka 20 amepata tatizo hilo wakati wa mazoezi siku ya ijumaa.


Muda huo wa miezi mitano ya matibabu,kutamfanya Barkley akose mchezo wa kufuzu michuano ya Euro 2016 ,wakati timu yake ya taifa ya England itakapomenyana dhidi ya San Marino pamoja na Estonia,mechi zitakazopigwa mwezi oktoba.

No comments:

Post a Comment