Laurent Koscielny
Aaron Ramsey
Kikosi cha
wabeba mitutu wa London Arsenal,kimeanza vema harakati zake za kuusaka ubingwa
wa ligi kuu ya England msimu huu,baada ya kuitandika mabao 2-1 Crystal Palace
na kuondoka na pointi zote tatu katika mchezo uliopigwa kunako dimba la
Emirates.
Kipindi cha
kwanza kilikuwa ni vuta nikuvute,na katika dakika ya 35 Crystal Palace wakapata
bao lililowekwa nyavuni na mchezaji Hangeland,kabla ya Arsenal hawajasawazisha
bao hilo katika dakika ya 45 ikiwa ni sekunde chache tu kabla ya kipindi cha
kwanza hakijamalizika,ambapo mchezaji Laurent Koscielny akaweka mambo kuwa sawa
kwa sawa.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi kila upande ukitaka kuibuka na ushindi,lakini upepo
ukawaendea vizuri wabeba mitutu,ambapo katika dakika ya 90 mchezaji Ramsey akaamsha
shangwe kwa mashabiki kwa kuandika bao la pili na la ushindi.
Ushindi huo
ni ishara tosha kwa kocha Arsene Wenger ambaye amekisuka vema kikosi chake
tayari kwa mapambano msimu huu.
Matokeo mengine,Leicester
imekwenda sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Everton,QPR wao wamekiona cha
moto baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Hull City,Aston Villa wameishikisha
adabu Stoke City kwa kuifumua bao 1-0,West Bromwich Albion nao wakienda sare ya
mabao 2-2 dhidi ya Sunderland,huku West Ham wakishindwa kutamba nyumbani na
kuruhusu goli moja kwa bila dhidi ya Totenham Spurs.

No comments:
Post a Comment