Saturday, August 16, 2014

KOCHA VAN GAAL, AANZA KUONJA CHUNGU ILIYOMSHINDA MOYEZ



            LUIS VAN GAAL
 
Manchester  United bado inaonesha haijakaa sawasawa tangu ilipotoka katika wakati mgumu msimu uliopita,kikosi hicho kikiwa chini ya kocha David Moyez aliyetimuliwa kwa aibu ya mwaka,na kikosi hicho kukabidhiwa kwa muda mikononi mwa Ryan Giggs.

Hali hiyo ya United ya kutia shaka kwa mashabiki wake,imeanza kujionesha leo katika patashika ya kuanza kwa ligi kuu Engalnd,baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya mashabiki dhidi ya Swansea City.

Vijana hao wakiwa ugenini walikitawala kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 28 likifungwa na mchezaji Kin Sung Young,na kuwaacha mashabiki wa United wakiwa hoi mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika.

Kipindi cha pili United wakajipapatua na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 53 likifungwa na mshambuliaji wao aliyetabiriwa kufanya makubwa katika msimu huu-Wine Rooney na kuamsha angalau shangwe kwa mashabiki wao.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa kocha Luis Van Gaal na vijana wake katika dakika ya 72,pale ambapo mchezaji wa Swansea Sigardsson,alipopigilia msumari wa mwisho kwa kuandika bao la pili na la ushindi,na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa United kulala nyumbani kwa mabao 2-1.

VIKOSI KAMILI KWENYE MCHEZO HUO:

UNITED: De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Lingard (Januzaj (24min), Fletcher, Herrera (Fellaini 67), Young; Mata; Hernandez (Nani 46), Rooney. Subs: Kagawa, Michael Keane, Amos, James

SWANSEA : Fabianski; Rangel, Amat, Williams, Taylor (Tiendalli); Ki, Shelvey; Routledge, Sigurdsson; Dyer (Montero 67), Bony (Gomis 77). Subs: Tiendalli, Montero, Tremmel, Bartley, Richards, Sheehan


No comments:

Post a Comment