Nimeamua kustaafu ,amenukuliwa Mertesacker akiteta na TV hiyo ya ZDF,ni jambo muhimu sana kwangu kustaafu kwa mafanikio kama haya baada ya kunyakua kombe la dunia huko nchini Brazil.
Ameweka historia ya kuitumikia ujerumani mechi 104,na sasa ameungana na wenzake kama Philip Lahm pamoja na mkongwe Miroslav Klose,ambao nao wameachana na majukumu hayo ya taifa tangu ujerumani ilipoinyuka Argentina bao 1-0 na kunyakua taji hilo la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990.


No comments:
Post a Comment