Mshambuliaji wa mabingwa wa kandanda wa England Manchester
City, Sergio Kun Aguero,amekubali kuongeza muda wa mkataba wake na sasa
utamfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2019,baada ya kusaini mkataba wa
miaka mitano.
Aguero,27-anaungana sasa na wenzake David Silva na Vicent Kompany kusaini
kandarasi ndefu ya miaka mitano,lakini anaungana pia na wachezajji wengine kama, Samir Nasri na
Aleksandar Kolarov,ambao nao wameongeza mikataba yao kusalia Etihad
Stadium.
Itakumbukwa Aguero,ameweka historia ya kufunga bao la dakika ya mwisho
ambapo City imefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya England,siku ya mwisho ya
kufunga msimu wa mwaka 2011/2012.
Amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 75 katika mechi 122 akiwa na klabu yake hiyo ya
Manchester City.
No comments:
Post a Comment