Kocha Manuelle Pelegrini akiwa na David Silva
vijana wa Man City wakisherehekea ubingwa wa England
Kiungo mshambuliaji David Josue
Jimenez Silva,ana ndoto za kunyakua taji la mabingwa ulaya,na ameiweka mbele Manchester
City kwamba ni moja kati ya vilabu vitakavyofanya hivyo na ndio maana ameamua
kuongeza mkataba wa miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Etihad.
Silva anakuwa mchezaji wa tatu kukubali
kuongeza mkataba mpya na mabingwa hao wa England,akitanguliwa na Samir Nasri na
Aleksandar Kolarov,na kuna taarifa kwamba wengine watakaoongeza mikataba yao na
Manchester City ni pamoja na Sergio Aguero na Vincent Kompany.
Silva ana historia ya kushinda
mataji mawili ya ligi kuu England, FA Cup na Capital One Cup tangu alipojiunga
na City kwa dau la pauni milioni 24 akitokea klabu ya Valencia miaka minne iliyopita.
Alikuwepo pia katika kikosi cha
Hispania kilichoshiriki michuano ya kombe la dunia iliyomalizika huko nchini
Brazil.

No comments:
Post a Comment