Javier Hernandez
Kocha Luis Van Gaal
Mshambuliaji wa Manchester United,
Javier Herndanez,anataka kuachana na klabu hiyo ya Old Traford na kujiunga na
klabu ya mabingwa wa Italia,Juventus Turin.
Taarifa za Javier kutaka kuondoka
United zimewekwa hadharani na kocha wa timu ya taifa ya Mexico,Miguel Herrera.
Mshambuliaji huyo ambaye amefunga
mabao 59 katika mechi 152 katika kipindi cha misimu mine akiwa na United,mbali
na Juventus kuwekwa kipaumbele cha kuhitaji huduma yake,lakini pia anawaniwa na
vilabu kama Inter Milan, na mabingwa wa Hispania Atletico Madrid pamoja na klabu ya England
Southampton.

No comments:
Post a Comment