kikosi cha wekundu wa msimbazi simba chini ya kocha Loga
Kocha Logarusic
Maswali yameanza
kutawala kila kona ya nchi hii kufuatia kitendo cha uongozi mpya wa klabu ya simba
chini ya Rais wake Evans Elieza Aveva,kumtimua kocha wao kipenzi Zdravko
Logarusic (Croatia),mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki wa
kusherehekea siku ya simba (simba day) ambayo hufanyika kila mwaka.
Uongozi huo
mpya ulituma maskauti wake kwenda nchini Zambia kuitongoza klabu ya Zesco
(wenye dhamana ya kuhakikish umeme wa uhakika unapatikana nchini Zambia) ili
kuja kucheza nao mchezo huo wa kirafiki na kuwapa raha mashabiki wake katika
maadhimisho ya simba day,huku wakijua fika kwamba klabu hiyo ni moto wa kuotea
mbali.
Uongozi wa
simba kupitia kwa makamu wake wa rais-muda mfupi tu baada ya kuingia
madarakani,ukatangaza kumuongezea kandarasi ya mwaka mmoja kocha Loga,kwa madai
kwamba wanaridhishwa na utendaji wake wa kazi licha ya kutoipa mafanikio
waliyokuwa wakiyahitaji.
Itakumbukwa
kwamba Loga awali aliingia mkataba wa muda mfupi (miezi 6) kumalizia msimu
akichukua mikoba toka kwa kocha Abdalah King Kibade Mputa pamoja na msaidizi
wake Jamhuri Kiwelo Julio Pereira Talantiin,wakati ambapo kikosi kikishikilia
nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kumalizika mzunguko wa kwanza wa ligi,na
tangu hapo kocha Loga akashindwa hata kwa bahati mbaya kuonesha mabadiliko na
kujikuta simba inamaliza katika nafasi hiyohiyo ya nne.
Mshabiki wa
simba wanajiuliza maswali:
1.kwanini kocha Loga amefukuzwa?
2.Iweje
simba ifukuze kocha kwenye bonanza?
3.Uongozi wa
simba walikurupuka kumpa mkataba mpya Loga?
4.Ninini hatima
ya simba katika msimu huu mpya wa ligi?
5.Kiongozi gani
aaminiwe na wanasimba kuchagua kocha?
6.Kamati ya
utendaji simba inajitambua?
Kama simba
imefukuza kocha mchana kweupe,je mpaka ligi inamalizika itakuwa imefukuza
makocha wangapi?
Haya ni
baadhi tu maswali yanayoulizwa na wanachama na mashabiki wa simba,maswali
ambayo bila kung’ata maneno,kupepesa macho wala kutikisa masikio-Aveva na
Kaburu wanawajibu wa kujibu.
NA KUNA TETESI KWAMBA PATRICK PHIRI-NDIYE KOCHA AJAYE SIMBA
NA KUNA TETESI KWAMBA PATRICK PHIRI-NDIYE KOCHA AJAYE SIMBA


No comments:
Post a Comment