Manchester
United imeongeza kitita chake nakufikia Euro milioni 50 kwaajili ya kumnunua
winga wa Real Madrid,Angel di Maria, 26.
Kocha Louis van Gaal pia anahitaji9
huduma ya beki wa klabu ya Ajax Amstardam ya uholanzi, Daley Blind, 24, pamoja
na kiungoi wa AC Roma, Kevin Strootman, 24.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger yupo tayari kufufua tena mazungumzo ya kutaka
kumsajili beki wa Liverpool ambaye hana uhakika na hatima yake ndani ya klabu
hiyo ya Anfeld, Daniel Agger, 29.
Hata hivyo
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers, amesema bado hajapokea maombi toka klabu
yeyote kuhusu usajili wa Agger.
Arsenal wanajipanga kurusha ndoano
zake kuwanasa mshambuliaji wa Germany, Lukas Podolski, 29, pamoja na
mshambuliaji wa Costa Rica, Joel Campbell, 22, ambao wote wanawindwa na klabu
ya Uturuki- Galatasaray.
Newcastle United
inaongoza mbio miongoni mwa vilabu vitatu kuiwania saini ya mchezaji kinda wa Manchester
United, Wilfried Zaha, 21.
Barcelona inataka kufanya usajili
madhubuti msiamu huu,na tayari imeanza kumfukuzia mshambuliaji wa zamani wa
Colombia anayeitumikia klabu ya Fiorentina, Juan Cuadrado,26 – ambaye ameripotiwa
kuwa United nao wanammezea mate.
Southampton
wanataka kumsajili beki wa kati wa klabu ya Steaua Bucharest , Florin Gardos,
25, nab ado wanamtolea macho beki wa kushoto wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno, Marcos Rojo,24.
Everton haijathibitisha
kwamba wanamuhitaji kwa mkopo winga wa Ghana,Christian Atsu, 22,kutoka Chelsea kwaajili
ya msimu huu.
Kocha wa Sunderland, Gus Poyet anaiota
mno huduma ya kiungo wa klabu yake ya zamani ya Brighton-Will Buckley, 24.

No comments:
Post a Comment