Thursday, August 7, 2014

KUFANYA VIBAYA KWA STARZ:WADAU WAZIDI KUMNYOOSHEA KIDOLE MALINZI


Wadau wa michezo wanazidi kumkalia kooni Rais wa shirikisho la kandanda nchini TFF,Jamal Emili Malinzi kuhusu kufanya vibaya kwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Starz ambayo imeondolewa katika msako wa tiketi ya kushiriki michuano ya mataifa ya afrika itakayofanyika mwakani kule nchini Moroco.

Wadau hao wametoa maoni yao wakati wakizungumza katika kipindi cha Malumbano ya Hoja kinachorushwa na kituo cha ITV,kilichokuwa kikijadili kuhusu Tanzania kufanya vibaya katika mashindano ya jumuiya ya madola iliyomalizika mjini Grasgow nchini Scotland na Tanzania kurejea mikono mitupu.

Kufanya huko vibaya kwa Tanzania,kumehusishwa pia na ubovu wa timu ya taifa ,Taifa starz,ambayo inasimamiwa na TFF na Malinzi akiwa ni rais wa shirikisho hilo.

wamesema Malinzi anahusika kwa kiasi kikubwa kufanya vibaya kwa Starz,kutokana na maandalizi yasiyokuwa yakitaalam ikiwa ni pamoja na kuiweka kambi timu hiyo mkoani mbeya ambapo kuna baridi kali wakati mechi ya marudiano ikipigwa msumbiji kwenye hali tofauti na mbeya.

No comments:

Post a Comment