Wakala wa mshambuliaji wa klabu ya PSG Edison Cavan,amethibitihsa kwamba
vilabu vya Arsenal na Liverpool,vimerusha ndoano ya kumuhitaji nyota huyo
haraka iwezekanavyo.
Awali Cavani aliripotiwa kuihama Paris Saint-Germain msimu huu, na kutimkia
kwenye ligi kuu ya England aidha kwenye klabu ya Manchester United au Chelsea,ambao
walikuwa wamekaa mkao wa kula kuinasa saini yake.
Hata hivyo,kwa mujibu wa wakala huyo Claudio Anelluci,amesema vilabu vyenye
nia ya dhati ya kumuhitaji Cavan ni Arsenal na Liverpool.
Wiki iliyopita Cavani alitamka wazi kwamba anajisikia furaha kuendelea
kuitumikia klabu yake kwa msimu mwingine,huku Liverpool wakimuwinda mshambuliaji wa Monaco-Radamel Falcao.

No comments:
Post a Comment