Klabu ya Inter Milan ipo tayari kumruhusu kiungo wake Fredy Guarin,
28, (Mcolombia) kwenda kujiunga na mashetani wekundu- Manchester United.
United pia ima matumaini ya kumpata
mlinzi wa klabu ya Roma - Mehdi Benatia, 27 kwa kitita cha Euro 30m,lakini
watalazimika kuingia katika mapambano na vilabu vya Chelsea pamoja na Real Madrid,ambavyo navyo vinahitaji huduma ya
Benatia.
Mabingwa wa Ebgland Manchester City,itakamilisha kabisa usajili wa beki wa klabu ya FC Porto Mfaransa Eliaquim Mangala kwa dau la Euro milioni 32,mwishoni mwa wiki hii.
Wabeba mitutu wa London Arsenal wamemgeukia kiungo mshambuliaji wa klabu ya Shakhtar Donetsk- Douglas Costa, 23,kutaka kumsajili baada ya kukwama kumsajili mchezaji wa FC Porto Juan Quintero, 21.
Daily Express
West Ham United inamuhitaji mshambuliaji wa Stoke City Peter Crouch, 33 – lakini wakitanguliza ofa ya Euro milioni 3 mezani.
Telegraph
Real Madrid wanataka kuwasajili magolikipa wa Chelsea, Petr Cech, 32, na Thibaut Courtois, 22.
Kocha wa Napoli ,Rafael Benitez,anataraji kupiga hodi kwenye klabu yake ya zamani Liverpool kujaribu kumsajili kiungo Lucas Leiva, 27.
Swansea wanajiandaa kumnyakua beki wa kati wa Napoli, Federico Fernandez,25.

No comments:
Post a Comment