Mshambuliaji wa klabu
yaMonaco ya Ufaransa Radamel Falcao,huenda akaihama klabu yake baada ya wababe
wawili kujitokeza kuhitaji huduma yake.
Falcao anahitajika sana
na Real Madrid ya Hispania pamoja na vijogoo Liverpool ya England,ambao kwa sasa wanapigana vikumbo kuona ninani
anayeweza kulamba dume kumsajili Mcolombia
huyo.
Kocha wa Liverpool
Brendan Rodgers,yeye anahitaji kumsajili Falcao kwa mkopo wa muda mrefu,huku
Madrid wakimuhitaji ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Wakati huohuo mchezaji
Loic Remy ameripotiwa kufeli katika zoezi la vipimo vya afya yake na hivyo
kushindwa kujiunga na Liverpool.
Hata hivyo Liverpool pia
imesitisha mpango wa kumsajili mchezaji wa Swansea City-Wilfried Bony.

No comments:
Post a Comment