Mshambuliaji karim
Benzema,amezitolea nje ofa za vilabu vya ligi kuu ya England kwa kuamua
kuongeza mkataba na klabu yake ya Real Madrid ya Hispania kwa muda mrefu hadi mwaka 2019.
Vilabu hivyo vya England
ni pamoja na wabeba mitutu wa London Arsenal,
Liverpool na Tottenham,ambao wamekuwa wakipigana vikumbo kuiwania saini yake.
Benzema amefanikiwa kufunga mabao
111 katika mechi 235 tangu alipojiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea
kunako klabu ya Lyon.
Miongoni mwa mabao hayo 24
ameyafunga katika msimu uliopita na kuiwezesha klabu hiyo kunyakua taji la
mabingwa barani ulaya.

No comments:
Post a Comment