Manchester United sasa
imekubali kutoa Euro milioni (£15m) kwaajili ya kumsajili mlinzi wa Arsenal, Thomas
Vermaelen,na kuiachia manyoya Barcelona ambao nao wanamuhitaji kwa udi na
uvumba.
Kocha wa United,
Louis van Gaal anataka kufanya usajili wa haraka baada ya klabu hiyo ya
mashetani wekundu kurejea toka katika ziara yao ya maandalizi ya ligi huko
nchini Marekani,na anataka kukamilisha usajili huo wa Vermaelen pamoja na mcezaji wa klabu ya Ajax-
Daley Blind kabla ya mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya Swansea City August
16.
Kwa upande wao Barcelona
wamesema wapo tayari kuweka mezani kitita cha Euro milioni (£10m) kwaajili ya
nyota huyo wa Ubeligiji.

No comments:
Post a Comment