Klabu ya Sunderland maarufu kama paka weusi,wamekamilisha usajili wa kiungo, Jack Rodwell toka klabu ya mabingwa wa England Manchester City.
Kiungo huyo wa England,23, amejiunga na Sunderland kwa ada ambayo haikuwekwa
wazi na kuingia mkataba wa miaka mitano.
"hii ni klabu ambayo inanifaa sana kuichezea” amesema Rodwell wakati
akihojiwa na mtandao wa Sunderland.
Rodwell alijiunga na Manchester City akitokea Everton kwa ada ya pauni
milioni 12 mwaka 2012,lakini ameshuka dimbani mara 26 kuitumikia klabu hiyo na
kufunga magoli mawili.

No comments:
Post a Comment