DONDOO ZA SOKA:MAGAZETI YA ULAYA AGOSTI 4,2014
KLABU YA Everton imeingiwa na hofu ya kumsajili winga wa Chelsea,
Christian Atsu, 22,kwa mkopo kutokana na mchezaji huyo kutopewa mechi nyingi na
klabu yake.
Liverpool na Tottenham wanapigana
vikumbo kutaka kujaribu kwa mara nyingine kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast ,Wilfried Bony, 25, na klabu yake
ya Swansea ipo tayari kumuuza kwa dau la pauni milioni £19m.
Daily Mirror
Beki wa Ubeligiji Thomas Vermaelen,
28, hana mpango wa kufanya mazungumzo juu ya mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal
ili kuishinikiza kumfungulia milango,na tayari vilabu vya Barcelona na Manchester
United,vipo tayari kumsajili kwa dau la pauni milioni £10m.
Tottenham ipo katika hatua za mwisho
za mazungumzo juu ya kumsajili kwa dau la pauni milioni £17m beki wa kati wa Argentina-Mateo
Musacchio, 23,toka klabu yake ya Villarreal na Spurs ipo tayari kumfungulia
mlango wa kutokea beki wake Younes Kaboul kwenda kujiunga na klabu ya Lazio ya
Italia,kwa dau la pauni milioni £6m.
Klabu ya Sunderland ipo tayari
kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto'o, 33,ambaye kwa sasa ni
mchezaji huru baada ya kutemwa na klabu yake ya Chelsea.
Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert anajipanga
kufanya mazungumzo na mlinzi wa Uholanzi Ron Vlaar, 29,ili kumpa unahodha wa
klabu hiyo.

No comments:
Post a Comment