Chicharitoooooooo
Shinjiiiiiiiii
Kocha wa Manchester United Mholanzi,
Louis van Gaal, amesema mshambuliaji wake Javier Hernandez,26 (Mexico) pamoja
na kiungo Shinji Kagawa,25 (Japan ),wanaweza kuuzwa kwenye klabu nyingine.
Taarifa toka ndani ya klabu hiyo ya
mashetani wekundu,zinasema Van Gaal atakutana na kumueleza makamu mwenyekiti
wa klabu hiyo, Ed Woodward kwamba Hernandez na Kagawa wanaweza kuuzwa, pamoja na
viungo Marouane Fellaini na Anderson,mshambuliaji Luis Nani,na hata kinda Wilfried
Zaha.
Kufuatia hali hiyo tayari klabu ya Atletico
Madrid wapo tayari kutoa kitita cha pauni milioni £25m ili kuzinasa saini za
mshambuliaji wa Mexico Javier Hernandez, 26, na kiungo wa Ki-Japan Shinji
Kagawa, 25.
Lakini hata hivyo kuna uwezekano wa Atletico
Madrid kufanya mabadilishano na United kwa kumtoa Ardan Turan ili wapewe Shinji
Kagawa.

No comments:
Post a Comment