Tuesday, August 5, 2014

XAVI HERNANDEZ:ASTAAFU KUITUMIKIA HISPANIA.


Kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Xavi Hernandez,amestaafu kuichezea timu yake ya taifa.

Xavi, 34 amefanikiwa kutwaa taji la dunia pamoja na mataji mawili ya ubingwa wa ulaya akiitumikia Hispania,na kuweka historia ya kulitumikia taifa hilo mechi 133, na kufanikiwa kufunga mabao 13.

  “ najisikia fuhara sana kulitumikia taifa lakngu kwa miaka yote niliyokuwemo,na kilikuwa ni kipindi kizuri mno kwangu kuitetea Hispania kimataifa”,amenukuliwa Xavi hii leo akizungumza mbele ya waandishi wa habari wakati akitangaza rasmi kustaafu.

Mashindano ya mwisho kulitumikia taifa lake ilikuwa patashika ya kombe la dunia iliyomalizika huko nchini Brazil hivi karibuni,na Hispania ikajikuta ikisukumizwa nje ya michuano hiyo baada ya kupokea kichapo kibaya cha mabao 5-1 dhidi ya Uholanzi na kichapo kingine cha mabao 2-0 mbele ya vijana machachari wa Chile.

No comments:

Post a Comment