Beki mpya wa klabu ya Bayern munich na timu ya taifa ya morocco
MEHNDI BENATIA amesema kuitumikia klabu hiyo ni ndoto yake ya muda mlefu na
amefurahi kupata nafasi ya kuwa chini ya Kocha PEP GUARDIOLA katika hiyo.
Mabingwa hao wa ligi ya bundesliga walithibitisha kuwa wamefikia makubaliano na klabu ya AS ROMA
ya nchini itali ya kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka 27 ,ambaye amesaini mkataba wa muda mrefu wa miaka mitano.
BENATIA aliekuwa beki muhimu katika klabu ya AS ROMA tangu ajiunge
na klabu hiyo akitokea klabu ya Udinese msimu uliopita, amekuja kuziba nafasi
ya JAVI MARTINEZ ambaye atakua nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuumia
kifundo cha mguu.


No comments:
Post a Comment